Hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa majengo ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Kampasi ya Mizengo Pinda, Katavi kupitia mradi wa HEET.
Aidha akielezea mradi huo mbele ya Mgeni rasmi katika hafla hiyo ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko, Makamu Mkuu wa Chuo cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Prof. Raphael Chibunda alisema mradi huo utagharimu kiasi cha takribani Shilingi Bilioni 17 za Kitanzania kwa ujenzi wa Majengo mawili ikiwa ni jengo lenye madarasa na Ofisi pamoja na bweni la Wanafunzi.
Kupitia mradi huo, Chuo kitaweza kupanua wigo wa udahili na kuwezesha vijana wengi zaidi wa Kitanzania kujiunga na masomo ya Elimu ya Juu.