Takribani shilingi bilioni 41 zimetolewa na serikali kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) unaofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Munngano wa Tanzania kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Benki ya Dunia kwa ajili ya ujenzi wa majengo mapya saba ya SUA ili kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuleta mageuzi makubwa katika utoaji wa elimu nchini.

Kati ya fedha hizo shilingi Bil 39.5 ni gharama za wakandarasi na shiringi Bil. 1.4 ni gharama za washauri waelekezi, ambapo katika Kampasi Mkuu ya Edward Moringe, chuo kitajenga majengo matano ambayo yataghalimu shilingi Bil. 19.2 majengo hayo yatahusisha jengo la taaluma litakaloweza kuchua watu 3500 kwa wakati mmoja.

Pia jengo la taaluma la Ndaki ya Uchumi na Stadi za Biashara litakalokuwa na ofisi za watumishi, vyumba vya semina na kumbi za mikutano zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 1000 kwa wakati mmoja, ujenzi wa maabara ya bioteknolojia, maabara jumuishi pamoja na maabara ya sayansi ya mimea vipando kwenye chumba.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mikataba  ya ujenzi kati ya Chuo kikuu SUA na wakandarasi  watakaojenga majengo hayo iliyofanyika Kampasi  Kuu ya Edward Moringe, Makamu Mkuu, Prof.  Raphael Chibunda amesema mradi huo unalenga  kuboresha mitaala kwa kuzingatia mahitaji ya soko la  ajira na kuongeza ubora wa usimamizi wa elimu ya  juu nchini hivyo mchango wa vyuo vikuu utaongezeka  kwenye uchumi wa taifa.

Amesema katika Kampasi ya Solomon Mahlangu chuo kitajenga majengo mawili yanayoghalimu shilingi Bil.17.1 ambayo ni jengo la taaluma lenye uwezo wa kuchukua watu 3500 kwa wakati mmoja na hostel yenye uwezo wa kuchua wanafunzi 500 kwa wakati mmoja.

Mhandisi Hanington Kagiraki ni mratibu wa mradi wa HEET kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia ameitaka SUA kusimamia vizuri ujenzi wa mradi huo ukamilike kwa wakati kama ilivyoainishwa kwenye mkataba kwa kuzingatia gharama za mradi na ubora wa kimataifa.